- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

PICHA: Kimbunga BEJISA Chasababisha Uharibifu Mkubwa katika Visiwa vya Reunion

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Reunion, Habari za Hivi Punde, Majanga, Mazingira, Uandishi wa Habari za Kiraia
Cyclone Bejisa by @delarue_julien on twitter [1]

Kimbunga Bejisa na @delarue_julien katika twitter

Januari 2, Kimbunga Bejisa kilisababisha uharibifu mkubwa katika kisiwa cha Reunion kilicho chini ya mamlaka ya Ufaransa. Mtu mmoja alifariki na wengine 15 kujeruhiwa vibaya, huku idadi ya nyumba zinazokadiriwa kufikia 82,000 zikiripotiwa kukosa huduma ya nishati ya umeme. Kimbunga hiki kimeshatulia na hali ya hatari imeshatangazwa kisiwani humo. Zifutazo ni picha nyingine zilizopigwa na raia waishio nchini humo:

http://www.youtube.com/watch?v=_mXLMJe7oKM [2]
Video ioneshayo kimbunga Bejisa katika Kisiwa cha Reunion. Video imewekwa na animax2013 katika mtandao wa Youtube.

Uharibifu uliofanywa na kimbunga Bejisa katika jiji la Mtakatifu Denis