- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Mwaliko wa Mapendekezo ya Tuzo za Blogu Nchini Kenya 2014

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Kenya, Teknolojia, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vyombo na Uandishi wa Habari

Waandaaji wa Tuzo za Blogu nchini Kenya 2014, ambao ni Umoja wa Wanablogu nchini humo (BAKE) [1]kwa sasa wanakaribisha mapendekezo ya wawaniaji wa tuzo hizo mpaka Februari 10, 2014. [2] Watumiaji wanaweza kupiga kura kwa njia ya mtandao kuanzia Machi 1, mpaka April 30, 2014 kupendekeza blogu wanazoona kuwa ni bora katika makundi 17 tofauti, ikiwa ni pamoja na kundi jipya la Blogu bora ya Afya na Blogu Bora ya Kaunti/Wilaya.

Bake logo

Nembo rasmi ya BAKE. Picha imetolewa: http://bloggers.or.ke.

Tuzo za Blogu nchini Kenya [3],  ni mradi wa  Umoja wa Wanablogu wa Kenya (BAKE) [4], wanakusudia kuwazawadia wnaablogu wanaobandika posti zao mara kwa mara, wenye maudhui sahihi na yenye kusaidia, wabunifu na wenye mambo mapya. Makundi mengine ni pamoja na: 

Hapa chini kuna video ya kuzinduliwa kwa Tuzo za Blogu Nchini Kenya:

Blogu zinaweza kupendekezwa kwa kutumia kiungo hiki [5].