- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Muandaaji wa Katuni ‘Meena’ Abadilisha Mitizamo ya Watu wa Asia ya Kusini Kuhusu Wasichana

Mada za Habari: Asia ya Kusini, Bangladesh, Afya, Elimu, Habari Njema, Habari za Hivi Punde, Haki za Binadamu, Maendeleo, Mahusiano ya Kimataifa, Mawazo, Sanaa na Utamaduni, Uandishi wa Habari za Kiraia, Utawala, Vijana, Wanawake na Jinsia
Screenshot from the cover of Meena Comic Book. Courtesy Unicef [1]

Picha iliyopigwa kutoka kwenye gazeti la Katuni za Meena. picha kwa idhini ya UNICEF

Ni miongo miwili tuu iliyopita,wanawake wengi wa nchi za Asia ya Kusini wamekuwa wakidhaeauliwa. wasichana wengi wa maeneo ya vijijini hawakuwa wakiruhusiwa kusoma. wasichana walizuiwa kuolewa pamoja na kufikia umri uliowaruhusu kuolewa, kwa maana hiyo hata masomo yangekuwa na faida gani? Majumbani, wavulana walipendelewa kwa kupewa vyakula vizuri, wasichana walikuwa wakipewa masalia ya vyakula.

Lakini, dhana hii ya ubaguzi imebadilika kwa kiasi kikubwa, kwa kiasi fulani, shukrani zimwendee mchora katuni [2].

Fanani wa kufirika Meena [3] ang,ara katika televisheni ya Asia ya Kusini inayorusha kipindi cha televisheni cha watoto kwa jina hilo hilo. Kwa ufadhili wa UNICEF [4], Meena na kipindi chake cha televisheni amekuwa maarufu sana katika eneo hilo. UNICEF iliandaa Mkakati wa Mawasiliano wa Meena (MCI) [5] kama mradi wa mawasiliano kwa umma uliolenga kubadilisha mitizamo ya watu inayoweka rehani uhai, ulinzi pamoja maendeleo ya wanawake wa Asia ya Kusini.

Bangladesh ilikwa nchi ya kwanza kukutana na Meena [6] mara baada ya filamu yake ya kwanza iliyokuwa inaonesha harakati zake za kutaka kwenda shuleni iliyokuwa ikioneshwa katika Televisheni ya Taifa ya Bangladesh(BTV) mwaka 1993. Waigizaji wengine katika simulizi zake ni pamoja na kaka yake na Meena ajulikanaye kwa jina la Raju pamoja na Kasuku ampendaye ajulikanaye kwa jina la Mithu.

Meet Meena. Image courtesy Wikimedia [7]

Kutana na Meena. Picha kutoka Wikimedia

Kwa mujibu wa taarifa ya zamani ya UNICEF [4]:

Tangu alipoanza, miaka 14 iliyopita, ameshawaonesha mamilioni ya wanawake na wasichana mambo wanayoweza kuyatimiza. Tayari ameshatoa mafunzo kuhusiana na mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto ya maneno ya dhihaka dhidi ya wasichana ikiwa ni pamoja na kukabiliana na changamoto ya fedheha ya ugonjwa wa Ukimwi kwa wasichanaShe has delivered messages on issues as far reaching as solving the problem of bullying through to challenging the stigma of HIV/AIDS through to girls’ right to play sport. Simulizi za Meena zinafurahisha na kuvutia sana, lakini pia, zinaakisi sana hali halisi ya maisha ya wasichana wanaoishi Asia ya Kusini.

Meena ameshatoa ujumbe wa kupinga ndoa za utotoni na utamaduni wa utoaji mahari, ikiwa ni pamoja na kupigia chapuo matumizi sahihi ya vyoo, kuwapeleka watoto wa kike shuleni, usawa wa kijinsia miongoni mwa watoto wa kike na wa kiume pamoja na haki ya elimu kwa wafanyakazi wa ndani. Vipindi vya televisheni anavyoviandaa vinaonesha mchango wa dhati wa wasichana katika jamii endapo watapewa nafasi.

Ni kwa namna gani ujumbe unaweza kusambaa kupitia katuni ndogo ya mtoto wa kike na kuwa na nguvu kubwa kiasi cha kuweza kudali mitazamo ya watu kwa haraka? Mama wa nyumbani, Naznin Rahman aliliambia gazeti la Daily Prothom Alo [8] [bn]:

আমার মা জোহরা বেগম তাঁর দুই ছেলের বিয়েতে যৌতুক নিয়েছেন। তখনো টিভিতে মীনা দেখাতে শুরু করেনি। তারপর যেই তিনি মীনা দেখতে শুরু করলেন, তাঁর চরিত্রে মেয়েদের প্রতি আলাদাভাবে একটা সহানুভূতি কাজ করতে লাগল। তারপর যখন তাঁর ছোট ছেলের বিয়ে দিলেন, তখনই আমরা বুঝতে পারলাম তিনি মীনার দ্বারা কতটা প্রভাবিত। আম্মা আমার ছোট ভাইয়ের বিয়েতে যৌতুক নেননি।

Mama yangu Zohra Begum alipokea mahari watoto wake wawili wa kiume. Wakati huo, Meena hakuwa akifahamika. Tangu alipoanza kumfuatilia Meena, alijijengea moyo wa huruma sana kwa wasichana. Hata mtoto wake mdogo kabisa wa kiume alipooa, tuligundua namna alivyofunzwa na Meena. Hakupokea mahari yoyote kutoka kwa bibi harusi kwa ajili ya kaka yangu mdogo .

Shuvo Ankur [9] aliandika katika ukurasa wa watoto wa BDNews24.com kuhusiana na mambo chanya aliyokwisha kuyagusia:

প্রচার হবার পর থেকেই মীনা পেয়ে যায় দারুন জনপ্রিয়তা। এবং এর ফলে আসতে থাকে বেশ কিছু পরিবর্তন। আগে গ্রামাঞ্চলে মেয়ে শিশুদেরকে স্কুলে যেতে না দিয়ে বাড়ির কাজ করানো হতো। মীনা কার্টুন প্রচার হবার পর থেকে আস্তে আস্তে ঘটতে থাকে পরিবর্তন। কারণ মীনা কার্টুনেও দেখানো হয়েছে যে তাকে স্কুলে যেতে দেয়া হতো না। কিন্তু কিছু ঘটনার পরে তাকে স্কুলে যেতে দেয়া হয়। এবং মীনা বিভিন্ন বুদ্ধিমত্তার পরিচয় রাখতে থাকে। সে লেখাপড়া শিখে তার বাবাকে ঠকে যাবার হাত থেকে রক্ষা করে। আবার বাড়ির গরু চুরি ঠেকায়। এমনি সব কাজের জন্য মীনা হয়ে যায় সবার জনপ্রিয় এবং সার্কভুক্ত দেশগুলোতে মেয়ে শিশুদেরকে অবহেলাও কমে যেতে থাকে।

Meena alipata umaaarufu tokea mwanzoni. Mabadiliko yalijidhihirisha punde baada ya kujulikana kwake. Mapema, katika maeneo ya vijijini, wanafunzi wa kike waliacha masomo na kuishia kufanya kazi za majumbani. Lakini hali ilibadilika mara baada ya vipindi vya televisheni vya Meena kuanza kuoneshwa. Kwenye televisheni, mwanzoni, Meena hakuruhusiwa kwenda shuleni kabisa. Lakini alibadililika sana na mwishowe alipata furasa ya kwenda shuleni. Ufahamu na uwezo wa Meena kiakili vilimuwezesha kujifunza kuhesabu pamoja na kujua maarifa mengine ya muhimu kwa ajili ya kumasaidia baba yake dhidi ya watu waliokuwa wakimdanganya. aliokoa ngombe wao kutoka kwa wezi. Uwezo wake kiakili ulifahamika na kila mmoja, na unyanyapaa dhidi ya wasichana katika nchi za Asia ya Kusini taratibu ulianza kupotea.

Sohanur Rahman [10] [bn] aliandika kwenye Kishorebarta kuwa, kuna mengi sana ya kujifunza kutoka kwenye kipindi hiki cha katuni:

[…] মীনার কাছ থেকে আমরা অনেক কিছুই শিখেছি। সেই ৯০ দশক থেকে আজকের দিন প্রযন্ত প্রায় ১৭ বছর ধরে মীনা আমাদের সমাজের প্রতিটি মানুষের মনের মনিকোঠায় একটি উজ্জ্বল চরিত্র হিসেবে স্থান দখল করে নিয়েছে।

Tumejifunza mengi kutoka kwa Meena. Tokea miaka ya 90 hadi sasa, Meena amekuwa maarufu sana na fanani wa kipekee sana katika jamii yetu.

Pia, Meena anatangaza redioni. Farzana Islam Tithi, mwenye umri wa miaka 24, ambaye anamtangaza Meena,aliliambia gazeti la The Daily Star [11]:

Kila mmoja alimpenda Meena tokea utotoni mwake, na kila mmoja bila kujali umri, aliangalia katuni zake kwa hamasa kubwa. Nami nilikuwa nikitazama kipindi hiki. Labda mtazamo wa Meena ulinikaa zana akili mwangu tangu awali na ndio maana ninaamini hisia hizi ndizo zilizonisaidia kumtangaza Meena.

Mtumiaji wa Twita, Bengalithings [12] alimtambua Meena kama kioo katika jamii:

Akaunti ya Twita ya UNICEF Bangladesh (@UNICEFBD [17]) ilikumbusha kuwa:

Kila mwaka Oktoba 24, “ Siku ya Meena [20]” inaadhimishwa nchini Bangladesh kuhamasisha jamii kuwaandikisha watoto mashuleni kwa asilimia 100, kukwepa wanafunzi kuacha masomo na kuhakikisha ilimu bora mashuleni.

Kwa mujibu wa taarifa [21] [bn], Meena amekuwa maarufu hata katika maeneo nje ya Asia ya Kusini. Kazi yake imeshanakiliwa kwa zaidi ya lugha 30 kama vile kiarabu, ki-Burma na kichina. Unaweza kupakua gazeti lenye hadithi za katuni za Meena hapa [22].