Kuokoa Maisha ya Tembo huko Laos

Photo from Facebook page of Elephant Conservation Center

Picha kutoka ukurasa wa Facebook wa Kituo cha Hifadhi ya Tembo

Laos hapo awali ilijulikana kama ‘ardhi ya mamilioni ya Tembo’ lakini hadi sasa idadi ya Tembo imeshapungua hadi kufikia mamia kadhaa kutokana na uwindaji haramu pamoja na biashara haramu ya pembe za ndovu. Baadhi ya tembo wanakufa kutokana na kufanyishwa kazi nyingi katika maeneo ya shughuli za ukataji na usafirishaji wa magogo.

Inakadiriwa kuwa tembo wa porini idadi yake inakadiriwa kuwa kati ya 300 hadi 600:

Wakiwa wametawanyika katika makundi madogo madogo, idadi ya tembo inaaminika kufikia 300 hadi 600. Kama ilivyo kwa nchi nyingine nyingi, Tembo wasiofugwa huko Laos, maisha yao huatarishwa na shughuli za kiuchumi za binadamu. shughuli hizi ni pamoja na ukataji miti hovyo, uwindaji haramu, upanuzi wa makazi ya watu pamoja na tembo kuuawa pale wanapoharibu mazao au kusogelea makazi ya watu.

Wakati huohuo, kuna zaidi ya tembo 420 wanaoshikiliwa:

Inasikitisha sana kwani idadi ya Tembo wanaoshikiliwa inazidi kupungua. Kiasi cha tembo wanaoshikiliwa waliosalia Laos kinakadiriwa kuwa ni Tembo 420.Sadly captive elephant populations are in decline. Only an approximate 420 remain in Laos. Kipindi cha milenia mpya, Tembo wamekuwa wakitumika kama sehemu ya kujipatika kipato, wamiliki wa tembo hawana budi kuwatumikisha tembo wao katika siku saba za wiki ili kujikimu kimaisha. Tembo hutumiwa zaidi kwenye shughuli za usafirishaji magoo, kazi ambayo ni ngumu na hatari sana kwa tembo. Tembo wa kike huchoka sana na kushindwa kuzaa na pia huweza kupoteza maisha katika kazi za usafirishaji wa magogo.

Kwa bahati nzuri, tayari kuna ufahamu wa umuhimu wa kuwatunza Tembo katika nchi hii. Miongoni mw makundi yanayopigia chapuo harakati hizi ni Kituo cha Hifadhi ya Tembo:

Kituo cha Hifadhi ya Tembo Kinajitofautisha na mashirika mengine ya utalii wa Tembo kwa kuwatunza Tembo kwa kuwajengea mazingira mazuri ya kuzaliana, uangalizi makini na wa karibu, matibabu na uchunguzi wa magonjwa mbalimbali. Usitegemee kuona watalii wakiwatumia Tembo hawa kwa siku nzima bila kupumzishwa!

Pia, kuna hospitali ya kwanza kabisa ya Tembo nchini Laos, ambapo pia, imekuwa ikitumika kama eneo la utalii la kutunza mali asili. Inatoa ushauri wa kitaalamu pamoja na namna bora ya kuishi na Tembo kwa watu wanaomiliki Tembo kwa ajili ya kujipatia kipato.

Kituo hiki pia kinatoa matunzo kwa Tembo waliojeruhiwa na kisha kuokolewa. Walishafanikiwa kumuokoa Tembo mdogo waliyempa jina la Noy. Baada ya miaka kadhaa kupita, tembo huyu atajitwalia jina jingine kupitia mchakato unaoelezewa na Afisa Mifugo afahamikaye kwa jina la Emmanuelle Chave:

Wakiwa na miaka mitatu, tembo hupata mafunzo kutoka kwa wamiliki wanaotarajia kuishi na tembo hao ya namna ya kupokea ishara mbalimbali ili kuweza kufanya kazi pamoja na binadamu.At three years old, elephants are trained by their future mahout, to respond different cues, in order to work with humans. Mzee wa kitamaduni husimamia safari hii, ambapo Tembo huacha maisha ya porini na kujiunga na maisha ya binadamu. Hadi mwisho wa mafunzo, tembo mdogo huzawadiwa miwa mitatu, ambayo juu yake kuna majina yaliyoandikwa. Jina katika mua wa kwanza atakaouchukua litakuwa lakwake.

Brita alitembelea kituo hiki na kugundua wajibu wake wa kutunza uhai wa Tembo:

Kituo cha Hifadhi ya Wanyama, bila shaka, ni moja ya maeneo machache unayoweza kuyatembelea na kujionea jinsi watu wanavyobadilika kulingana na vionjo na matakwa ya Tembo na siyo Tembo kubadilika kulingana na namna watu wanavyoishi.

Linapokuja suala la kuchagua niende kwenye sehemu ipi ya utalii wa Tembo, huwa ninakuwa na machaguo mengi kwani karibu maeneo yote ulimwenguni huwa na tabia ya kutokuwajali kabisa tembo, ikiwa ni sawa tu na kuhama kutoka kushuhudia maisha mbaya kabisa ya tembo (= kusafirisha magogo) kwenda kushuhudia maisha mengine ya tembo(= kutokutunzwa vizuri kunakotokana na shughuli za kitalii).

jo ebisujima pia alihunduria kituo hiki na kujifunza kuwa, kuweka kiti mgongoni mwa tembo ni maumivu makubwa kwa mnyama huyu:

Miongoni mwa mambo ya muhimu niliyojifunza ni kuwa, viti vilivyoko migongoni mwa tembo vinavyotumika kubebea watu na mizigo kwa hakika si sahihi kabisa kwa wanyama hao. Hii ni kwa sababu ya namna mifupa yao ilivyojengeka. Ni nafuu sana kwa Tembo kutembea bila aina yoyote ya mzigo na wala kuwekwa juu ya shingo zao.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.