Wito wa Maombi ya Mradi – Ufadhili wa Maktaba za Umma wa EIFL

Banner FINALMaktaba za umma na zile za jamii katika nchi zinazoendelea, zenye uchumi wa mpito, zinakaribishwa kuwasilisha maombi ufadhili wa Mradi wa Kuboresha Maktaba za Umma unaoendeshwa na shirika la EIFL. Maombi yanayoweza kukubaliwa ni yale yanayokusudia kubuni huduma mpya zitakazotumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa njia za kiubunifu ili kuweza kukidhi mahitaji ya watoto na vijana katika jamii zao. Waombaji wanaweza kutuma ‘andiko’ la mradi unaoweza kugharibu hadi Dola la Kimarekani 20,000.

Miradi iwe na sifa zifuatazo:

  • Itumie mbinu za kiubunifu kujaribu kuyakidhi mahitaji ya watoto na vijana, na
  • Itumie teknolojia ya kidijitali katika mbinu mpya na zenye ubunifu, na
  • Ilenge kufanya kazi kwa ushirikiano na idara au mashirika ya serikali, mashirika ya kiraia au wabunifu wa teknolojia.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea tovuti ya EIFL kujua masuala muhimu kama gharama zinazotarajiwa, vigezo vya uteuzi, ratiba, dondoo za waombaji watakaofanikiwa, na mengineyo.

Tarehe ya mwisho kuwasilisha maombi ni Januari 31, 2014.

1 maoni

  • BAHATI METHOD

    Karadea ni shirika lisilo la kiserikari lakini inayo makitaba ya jamii, sasa mnaweza kusaidia ili iweze kuendelea mbele.

Sitisha majibu

jiunge na Mazungumzo -> BAHATI METHOD

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.