Wanaijeria Wamkumbuka Nelson Mandela

Nelson Mandela, rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini aliyehusika kwa kiasi kikubwa katika mapambano ya kuubomoa ukaburu, alifanriki Alhamisi, Decemba 5, 2013 akiwa na umri wa miaka 95. Mtu huyo anayependwa sana, na Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, anayejulikana pia kama Madiba, alitumikia kifungo cha miaka 27 jela alikokuwa amefungwa kwa sababu ya harakati zake za kisiasa wakati wa utawala wa makaburi nchini humo kabla ya yeye kuwa Rais.

Tangu habari za kifo chake zifahamike, Wanaijeria wamekuwa wakiadhimisha maisha yake na nyakati za mtu huyo anayesemekana kuwa tunu kubwa kuliko zote kwa mwanadamu ambayo Afrika imewahi kujaaliwa. Katika mtazamo wa Afrika duniani, kuondoka kwa jemedari huyo si wakati wa kuomboleza, bali wakati wa kutafakari na kufurahia kumbukumbu yake. Tanzia zimekuwa zikimiminika katika mitandao ya kijamii ya Naijeria tangu kutangazwa kwa kifo chake. 

Nelson Rolihlahla Mandela alikuwa rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini Afrika Kusini. Picha imetolewa na South Africa The Good News chini ya leseni ya Creative Commons (CC BY 2.0).

Oluwatosin Olaseinde, mhasibu na mkaguzi wa mahesabu, alipata haya kwa ufupi:

“Leo haipaswi kuwa siku ya maombolezo, yapaswa kuwa maadhimisho. Mandela aliishi maisha makuu, alikula chumvi, Apumzike kwa Amani

Oby Ezekwesili, makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, kanda ya Afrika, aliandika:

Itakuwa safari ndefu kwa watawala wengi wa Afrika kurithi TUNU YA ASILI ya #Madiba. Watakuwa watu wa maana wale wote watakaothubutu kuchukua hata hatua ya kwanza tu!

Twitter user @ba55ey celebrated Mandela: 

Alikuwa hamasa kwa watu karibu kila nchi ya dunia #Madiba

Mwandishi wa Habari Abang Mercy-Asu aliweka video ya Madiba ya “Hotuba ya Uhuru”:

VIDEO: Hotuba ya Uhuru ya Nelson Mandela http://t.co/tYblZ45j3y — Abang Mercy-Asu (@AbangMercy)

Mwandishi na Mwanablogu Nze Sylva Ifedigbo aliweka posti hii kwenye blogu yake:

Siku nzuri ya kuweka kumbukumbu hii >> KUJIFUNZA KUTOKA KWA MTU ANAYEPENDWA ZAIDI DUNIANI#NelsonMandela | Nzesylva's Corner http://t.co/4AYcPPp7uU — Sylva Nze Ifedigbo

Mtumiaji  @KwamiAdadevoh alitoa wito kwa tafakuri za kila mtu mmoja moja: 

Nimekaribia umri ambao #Madiba alikuwa nao wakati anawekwa gerezani. Kimwili na kiakili hivi kweli ningeweza kuhimili miaka 27 na bado nikaweza kuleta mabadiliko duniani?

Mtumiaji @WilDeji, mkufunzi wa mbwa, alijaribu kukumbuka siku ya kihistoria Madiba alipoachiwa kutoka gerezani: 

“Wamemwachia Mandela” -unakumbuka wakati huo uliposikia habari hizo? Ulikuwa wapi na ulikuwa unafanya nini…?#Madiba

Bola Ahmed Tinubu, mwanasiasa na Mpinzani maarufu Naijeria, akasema: 

Watawala wanamsherehekea Mandela, lakini hawana nidhamu yake na muono. Wanasimama kuziba njia za watu wao na kuifanya Afrika ionekane kituko.

Nnayelugo alitoa wito wa kile alichokiita “U-Mandela”:

Wanaijeria wapaswa kuanza kwanza (kwenye njia ya “Umandela”) kwa kwenda kazini kwa wakati

Maneno yaliyoonekana kuwa ya ukosoaji katika twiti ya mtumiaji wa mtandao wa twita anayejiita Load of the Gourds yalikuwa na kejeli:

“Kiongozi” yeyote wa Naijeria atakayeonekana kumwaga machozi ya mamba kwa ajili ya Mandela alazima afungwe miaka 14 katika jela ya Kirikiri [Gereza lenye ulinzi imara kabisa mjini Lagos, Nigeria]

Mtumiaji @nnamdiarea hakuwaonea huruma watawala wa Afrika:

Kitu kibaya kuhusu kifo cha Mandela itakuwa ni hotuba ndefu, zisizona msisimko wowote kutoka kwa watawala wa Afrika ambao wanataka kumsifu lakini hawana mpango wa kujifunza kutoka kwake. -Kero

Machambuzi wa mambo ya kijamii Jason Kayode alifikiri kwamba si jambo la msingi sana kujaribu kuwafananisha viongozi na Mandela kuliko ilivyo kwa raia kujifananisha naye:

Swali: Kiongozi gani wa Naijeria anaweza kuwa kama #Madiba. Jibu: RAIA yupi wa Naijeria anaweza kuwa kama #Madiba
RamblersINC, a mwanablogu na Mwanafasihi, alijumuisha kumbukumbu ya Madiba:

Somo hapa ni kwamba jina jema ni bora kuliko ukwasi, umaarufu au madaraka. Thamani ya maisha ya mtu haiko katika umiliki wa mali.

Mojisola Sodeinde aliandika: 

Leo amekuwa maarufu kuliko waliomfunga, juu sana kuliko viongozi wote wa dunia, juu sana ya ufalme, akiwa marehemu Nelson Mandela ni mkuu kuliko maisha

Molara Wood (@molarawood), mwandishi, mwanahabari na mhariri, alihitimisha hisia za wa-Naijeria katika twiti hii ya kishairi:

Mandela ameenda zake. Jua limechwea. Tembo amelala. Zaidi ya Maneno. Kwa heri, Madiba. Nenda salama

Madiba atacheza kwa mrindimo wa wimbo huu wa maombolezo, umeandikwa na mshairi wa ki-Naijeriat, Tosin Gbogi, anapokaribia “lango la mbinguni”: 

Nelson, mwanga angavu uliomwulika giza
Miaka mingi iliyoshiba kumbukumbu,
Lugha yakwama mpaka kisigino cha mwisho

Soweto yakumbuka mipaka ya adhabu ya mapinduzi
Usiku kama huu, Nelson, usiku kama huu ambapo
Miale ya mwanga iliyomwulika dunia nuru ya
Kumbukumbu: mauaji makubwa
Na ubaya: Botha akiwa imara dhidi ya wasio na akili
Usiku katika midomo yake, alitamka rangi yake kuwa adui wa
Mawio yaliyokileta Kisiwa cha Robben kwenye magoti yake.

Yu njiani, Nelson hatimaye yu njia kwenda kwenye Mji wa Uhuru
Na akawe na amani ya milele, oh
Malaika Biko na Brutu, waharakishe kuingia kwake kwenye lango la mbingu

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.