Kitendo cha kijana mmoja kupigwa risasi Novemba 23, 2013 kwenye treni ya Moscow kimeibua mjadala mpya mtandaoni kuhusu harakati zenye msimamo mkali Urusi kubagua wahamiaji nchini humo. Tukio hilo lilirekodiwa kwenye kamera za CCTV nadani ya treni hiyo. Kwenye video hiyo mwanaume mmoja anaonekana kusogelea abiria wawili waliokuwa wamekaa na baada ya kubishana kidogo, mmoja wa wanaume hao anasimama, anainua pastola yake angani na kumpiga risasi mtu wa kwanza kwenye paji la uso akiwa karibu kabisa nae. Mwenzake, kijana mdogo, naye anaitoa bunduki yake na kuiweka kwa majeruhi huyo, wakati wawili hao wakitoroka. Video hiyo[ru] ilipatikana kwa juhudi za gazeti la LifeNews, na tangu wakati huo imekuwa ikisambaa mno kwenye mitandao ya kijamii nchini Urusi.
Majeruhi wa risasi hiyo alikuwa Hashim Latipov, raia wa Dagestan, wakati wanaume hao wawili waliompiga risasi, wanaonekana bila sababu yoyote, kuwa Warusi wabaguzi wa rangi. Na ingawa Latipov anasema kwamba mabishano hayo hayakuanzia kwake, lakini ukweli kuwa rangi yao ilikuwa sababu tosha kwa Wahafidhina wa Kirusi kudhania kuwa wa-Rusi hao wawili walifanya hayo katika jitihada za kujilinda. Sio hayo tu, bali hata kinachoendela kufanywa na jamii ya wahafidhina mtandaoni hivi sasa ni yale yale ya kutetea uhalifu –watu hao wawili wanajengewa taswira ya kuwa walinzi wanaojihami dhidi ya vurugu za wageni.
Mtazamo wa walindi wanaopambana na uhalifu (usijali, maana wala si kweli) unakubwa na picha kama hii hapa chini, ambapo wapiga risasi hao wawili wametengenezwa kwa programu ya kompyuta kuwa tangazo la filamu “Watakatifu wa Boondock.”
Mtazamo kama huo wa kuwafanya wahalifu hao kuonekana kuwa “hawakuwa na neno” umewekwa kwenye mjadala mwingine –hapa pakiwa na vichwa vya watu hap kutoka kwenye filamu ya Quentin Tarantino iitwayo Pulp Fiction ikatengeneza na kompyuta ili ionekane kuwa video ya kamera za CCTV:
Lakini picha nyingine kutoka kwenye video hiyo hiyo inaonekana kuwa inajitosheleza bila kuhitaji kutengenezwa kwa programu za kompyuta —imekuwa mchoro wa sanaa:
Mwingine alimpaka rangi mmoja wa wahalifu katika michoro ya ki-Orthodox, ili apewe hadhi ya kidini, labda alifanya mchezo wa kuifananisha na filamu ya Watakatifu wa Boondock:
Picha hiyo ilimfanya mwanablogu mmoja wa VKontakte kujibu [ru]:
Такой воодушевленной “народной канонизации” не было уже очень давно… да чего там давно — вообще ничего подобного на своем веку не припомню, если честно.
Haijawahi kutokea hamasa ya kitendo cha “kufanya kitu cha hovyo kiwe kitakatifu namna hii” kwa muda mrefu sasa —Sijawahi kuona kitu kama hiki maisha yangu yote.
Vyovyote iwavyo, mambo kama haya yanaonyesha picha halisi ya matatizo ya ubaguzi wa rangi unaozidi kushika kasi nchini Urusi.