- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Misri: Kampeni kwa Ajili ya Haki za Watu Wenye Mahitaji Maalum

Mada za Habari: Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Misri, Afya, Haki za Binadamu, Maendeleo, Sheria, Uandishi wa Habari za Kiraia, Utawala, Vijana

Wamisri pembezoni wenye mahitaji maalum wamekuwa wakifanya maandamano kwa haki zao kabla na tangu mapinduzi ya #Jan25. Hata hivyo, malalamiko yao bado hayajatatuliwa. Wakati Kamati ya watu 50 wanapiga kura juu ya rasimu ya hivi karibuni zaidi ya Katiba ya Misri, kampeni ya Zayee Zayak, ambayo hutafsiriwa kuwa “Mimi ni kama wewe” lugha ya Kiarabu cha Misri kisicho rasmi, ilianza katika Misri kwa lengo la kuongeza uelewa juu ya haki za kikatiba za watu wenye mahitaji maalum katika nchi.
Sensa ya 2006 ilionyesha [1] kuwa karibu Wamisri milioni walikuwa na aina fulani ya ulemavu, lakini mashirika yasiyo ya kiserikali yenye ari na mashirika ya kimataifa yanakadiria [2] kuwa idadi yao haipungui milioni 8.5. Wanaharakati wa Zayee Zayak wanathmini kwamba Wamisri wapatao milioni 17 wanayo mahitaji maalum:

Unaweza kufuata mijadala kupitia kundi lenye ari, ‘Uelewa wa Ulemavu katika Jamii za wa-Misri’ [3] (En).