- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

“Mimi ni Mchuuzi Mjerumani Mjini Dakar”

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Ulaya Magharibi, Senegali, Ujerumani, Elimu, Habari za Wafanyakazi, Maendeleo, Mawazo, Safari, Sanaa na Utamaduni, Uandishi wa Habari za Kiraia, Ubaguzi wa Rangi, Uchumi na Biashara

Muda mfupi baada ya kuwasili kwangu Senegal, nilikutana na kijana. Alinieleza hamu yake ya kuondoka Senegal katika mkutano wetu wa kwanza. Nilitaka kuelewa yaliyosababisha hamu yake ya kuondoka na hali ya maisha yake ya kila siku ili nipate kufahamu maelezo ya kijamii na ya kiutamaduni ya kutaka kwake kuondoka. Alikuwa mchuuzi. Kwa hivyo, siku moja nikamwomba ruhusa niandamane naye ili nimtazame akishughulikia pilkapilka zake za kawaida, naye akakubali. Kwanza, akanizungusha mitaani nikiuza bidhaa zake, eti nipate mafunzo. Aliifurahia faida aliyoipata [ ..] Kazi yangu mpya ikanipa uelewevu bora zaidi wa sekta isiyo rasmi nchini humu. Inajulikana kama “door waar,” na ina umuhimu wa kimsingi katika maisha ya vijana Wasenegal. [ ..] Mara nyingi nilikabiliana na mshangao kuhusu asili yangu. Watu wengi sana hawakuamini kwamba mzungu angeweza kushughulikia kazi za aina ile nchini humu. Mara kadha, watu walidhani kwamba nilikuwa mwaminifu kuliko wachuuzi wengine, na bidhaa zangu zilikuwa bora kuliko zao. Ilionekana kama kwamba watu wengi walidhani kuwa bidhaa za mwuzaji mzungu lazima ziwe za hali ya juu.

Kuwa mchuuzi mitaani si kazi rahisi, hasa nchini Senegali. Hata hivyo hilo ndilo chaguo alililofanya Sebastian Prothmann, Mjerumani asilia, baada ya kuwalisi Dakar, Senegal miezi michache iliyopita. Video hii inamwonesha Prothmann akiwa kazini[fr]:

Prothmann anaeleza katika mahojiano na blogu ya Dakaroiseries namna alivyojikuta akifanya kazi hii isiyo ya kawaida [1] [fr] katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi:

Au début de mon séjour j’ai rencontré un jeune homme qui a lors de notre premier contact manifesté son désir ardent de quitter le Sénégal. J’étais curieux de comprendre son ‘’monde vécu’’ pour aboutir à des interprétations socio-culturelles sur  son envie  d’émigrer. Il était marchand ambulant. Donc, un jour je lui ai demandé si je pouvais l’accompagner dans sa routine quotidienne. Ce qu’il a accepté. Il m’a donc fait faire un premier tour, soi-disant pour mon apprentissage.  Il en  était réjoui, car on a fait de bons bénéfices [..] Avec cet engagement, j’ai eu plus des prises de conscience dans le secteur informel, communément appelé aussi « Dóor waar », qui joue un rôle fondamental pour la jeunesse sénégalaise. [..] j’étais souvent confronté à une incrédulité frappante quant à mes origines. La plupart des personnes n’ont pas cru qu’un homme blanc peut s’investir dans un tel travail. Plusieurs fois j’étais aussi confronté à une confiance plus élaboré á mon égard. Il y avait des considérations selon lesquels moi en tant que Blanc devait vendre des produits de bonne qualité.