Mandela na Mao, Hawakushabihiana sana.

Jeremiah kutoka katika studio ya Granite atoa maoni yake kwenye Televisheni ya Taifa ya China, CCTV akitaka kuonesha uhusiano uliokuwepo kati ya Mandela na Mao Zedong:

Mandela hakushabihiana sana na Mao. Mao alikuwa muumini wa udhanifu kama tafsiri ya neno linavyotanabaisha, mtu aliyeamini kuwa, mchakato wa utendaji wa jambo ndilo jambo la msingi sana kuliko matokeo yake, mara nyingi hata kama matokeo yanakuwa mabaya. Katika harakati zake, Mandela mara zote alikuwa akipigania usawa. Mara nyingi alionesha utayari wake wa kutumia mbinu mbadala za kuhakikisha ndoto yake ya usawa nchini Afrika Kusini inafikiwa.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.