- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Kimbunga Haiyan: Hadithi ya Ujasiri Kupitia Filamu Fupi

Mada za Habari: Asia Mashariki, Ufilipino, Maendeleo, Majanga, Mwitikio wa Kihisani, Uandishi wa Habari za Kiraia

Kimbunga Haiyan [1], filamu fupi kwa hisani ya Janssen Powers, [2] inaonyesha hali baada ya dhoruba ambayo mapema mwezi Novemba iliua zaidi ya watu 6,000 katika jimbo la Philippine la Leyte.

“Kwa kawaida, mimi nia yangu ilikuwa kupata habari za uharibifu huo, “Powers aliandika katika maelezo ya kazi yake. “Nilicho pata hata hivyo, ilikuwa habari ya ujasiri.”

Katika maandishi, picha za maafa ni mbadala na mahojiano na waathirika, ambao wanajadiliana juu ya janga na kutazamia siku zijazo.

Kwa hadithi zaidi juu ya Kimbunga Haiyan angalia hapa [3].