Kampeni ya “Kabila Langu ni Sudan Kusini” na “Mimi Nachagua Amani”

Kufuatia mgogoro ambao umeliandama taifa jipya kabisa duniani, Sudan Kusini, tangu Desemba 16, 2013, taifa hillo na marafiki wa watu wa Sudan Kusini wamekuwa wakiendesha kampeni katika mtandao wa twita kwa jila la #MyTribeIsSouthSudan na #iChoosePeace kutoa mwito wa amani na umoja katika nchi hiyo.

Sudan kusini ilipata uhuru Julai 9, 2011 baada ya kura ya maoni ambayo ilifanyika siku ya uhuru kutoka Sudan kupitishwa.

A South Sudanese girl at independence festivities

Msichana wa Sudan Kusini kwenye sherehe za sikukuu ya uhuru
Picha ni kwa matumizi ya umma – iliwekwa mtandaoni mwanzo na Jonathan Morgenstein/USAID kwenye flickr

Zifuatazo ni baadhi ya jumbe kwenye mtandao wa Twita kuunga mkono amani na umoja wa kitaifa:

Mimi si mwanasiasa, siko jeshini, sifanyi kazi serikali, ni kwamba ninachagua amani kwa nchi yangu

Ninaomba kusitishwa kwa kwa hiki kichaa…kusitishwa kwa utengano..tusimame wa wananchi wa Sudani ya Kusini

Haimaanishi sisi hatuna makabila, ila tu kwamba sisi ni wamoja, yaani wananchi wa Sudani Kusini

Nchi yangu na watu wke, usalama wao ni muhimu zaidi kuliko tamaa za kuridhisha nafsi kwa wanasiasa

Huu ndio wapaswa kuwa ujumbe. Acheni kupigana na ndugu zenu kwa ajili ya maslahi ya kisiasa kwa watu fulani

South Sudan's Vice-President Riek Machar is seated in his office, June 30, 2012

Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Sudan Kusini Riek Machar anatuhumiwa kwa mipango ya kuipindua serikali.
Picha kwa matumizi ya umma – Voice of America

Ninakataa kuanza kumbia kimbia kwa mara nyingine, ninasema HAPANA kwa vita nyingine

Tukumbuke siku zote kuwa serikali inatutumikia, na sio kinyume chake! Piganieni amani

Baada ya miaka yote ya kuumizana, kwa nini tuendelee kufanyiana mambo haya?

Vita ndicho kinachoigawa Sudani yangu, hatutaki vita tena Sudani sasa. Ninaunga mkono kampeni ya Kabila langu ni Sudnai Kusini

Makabila yote 64 yanatoa wito kwamba Kabila Letu ni Sudani Kusini na Ninachagua Amani

Vita ndicho kinachoigaw aSudani yangu, hatutaki hayo yatokee nchini humu sasa. Ninaunga mkono kampeni ya Kabila Langu ni Sudani Kusini na ile ya Ninachagua Amani

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.