- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Cuba: Madiba Alifanya Mengi Mazuri Pamoja na Mapungufu Aliyokuwa Nayo.

Mada za Habari: Nchi za Caribiani, Cuba, Haki za Binadamu, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza

Blogu ya Cuba Without Evasion [1] yatanabaisha kuwa, namna pekee ya kumuenzi Nelson Mandela ni kwa “kuiga mfano wake wa kusamehe na Usuluhishi”:

Ninakusamee…kwa urafiki uliokuwepo kati yako na…dikteta aliyekuwa muovu kiasi ambacho watu wangu hawakuwahi kuushuhudia…kwa kuweka mkono wako– kwa ajili ya kuwaokoa watu wako- kwenye mabega yavujayo damu ya yule aliyenitenga na kunilaani mimi.