Wimbi la Ukatili Dhidi ya Waandishi wa Habari Nchini Guatemala

Mwandishi wa habari wa Guatemala Carlos Alberto Orellana Chávez alipigwa risasi mnano Jumatatu Agosti 19, 2013, yeye ni mwandishi wa habari wa nne kuuawa nchini Guatemala mwaka huu.

Katika makala ya maoni [es] iliyochapishwa katika gazeti la Guatemala Prensa Libre, mwandishi maalum wa ripoti ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya uhuru wa kujieleza Frank La Rue alishutumu “wimbi la hivi karibuni la ushambulizi dhidi ya waandishi nchini,” kama Alejandro Martinez anavyoripoti katika Uandishi wa Habari wa The Knight Centre katika blogu ya Amerika:

La Rue alikosoa utawala wa Rais Otto Perez Molina kwa kushindwa kuzuia uhalifu nchini, kipendeleo kwa maslahi binafsi, kutesa viongozi wa kijamii na kutolinda waandishi wa habari kutoka unyanyasaji wa mahakama, kesi za kisheria, vitisho, ushambulizi wa kimwili na mauaji.

“Leo vurugu imegeuka kuelekea sekta ya vyombo vya habari ambayo inashikilia nafasi muhimu kuelekea wale walio katika madaraka, kwa sababu ya kazi yao ya kijamii ya kuchunguza na kutoa taarifa, lakini kiwango cha mwaka huu cha ushambulizi hakijaonekana katika muongo mmoja,” alisema La Rue, ambaye alielezea vurugu kama “hatua ya nyuma kwa ajili ya demokrasia na (nchi) mchakato wa amani.”

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.