- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Wanasayansi Kutoka Duniani Kote Wakusanyika Nchini Brazil

Mada za Habari: Amerika Kusini, Brazil, Maendeleo, Sayansi, Uandishi wa Habari za Kiraia, Utawala
World Science Forum [1]

Kongamano la Dunia la Sayansi

Jukwaa la Sayansi Duniani [2] (WSF) linajumuisha mamia ya wanasayansi kutoka duniani kote wiki hii nchini Brazil, kujadili wajibu wao katika karne ya 21 na kusisitiza umuhimu wa ushauri wa kisayansi katika maamuzi ya kisiasa na kiuchumi.

Brazil imekuwa mwenyeji wa matukio kadhaa ya kujadili kuondoa umaskini na maendeleo endelevu kutoka katika mtazamo wa makundi mbalimbali ya kijamii, mara kwa mara maadui, kama vile Rio +20 [3], na mkutano wa watu [4] na Kongamano la Kijamii DunianiMtandao [5] katika lugha ya Kiingereza, lugha rasmi ya tukio hilo, na itajumuishwa katika mitandao ya kijamii kupitia alama ashiria #WSFBRAZIL.