Mnamo tarehe 30 0ctoba, watu 87 waliokuwa wakijaribu kuifikia bahari ya Mediterania walifariki mara baada ya madereva waliokuwa wakiendesha magari waliyoyatumia kusafiria kuwatelekeza wahamiaji hao katika Jangwa la Sahara. Wahamiaji hawa walihangaika kutafuta msaada bila ya mafanikio. Simulizi ya kuhuzunisha kutoka kwa mmoja wa watu walionusurika aliyejulikana kwa jina la Shafa mwenye umri wa miaka 14, yaelezea taabu wanazokumbana nazo wahamiaji wengi wanaojaribu kwenda Ulaya na vikwazo wanavyokabiliana navyo. Kwenye makala iliyopewa kichwa cha habari “Kifo katika Safari ya Kuelekea Ulaya”, Philippe Rekacewicz, ambaye ni Mfaransa na msanifu wa ramani, atoa ufafanuzi unaoambatana na mfululizo wa ramani kuhusiana na harakati za wahamiaji kutoka Afrika kuelekea Ulaya.[fr]:
1 maoni