Wa-Malawi Wajiandae kwa Kashfa Zaidi za Ufisadi

Steve Sharra anaelezea kwa nini Wamalawi wanakabiliwa na kashfa ya zaidi za ufisadi baada habari kuwa wazi kwamba baadhi ya wa-Malawi wenye nguvu walitumia vibaya Mfumo wa Pamoja wa Ndani wa Udhibiti wa Fedha kupora mabilioni ya fedha za umma:

Kutokuwepo kwa usawa wa kijamii kunajenga ufa mkubwa miongoni mwa Wamalawi, jambo ambalo ni bomu linalosubiri kulipuka. Kuongezeka kwa matukio ya matumizi ya nguvu na uharibifu tunaoshuhudia nchi kote kila siku ni tone dogo katika bahari ya hasira na chuki inayotokana na kukosekana kwa usawa huu. Hali inafanywa kuwa ngumu zaidi na namna vyama vyetu vya kisiasa visivyo na njia imara za kuendesha harambee ya kuchangiwa fedha kwa ajili ya kuendesha shughuli zake, hali inayosababisha uwanja wote wa kisiasa kuwa vurugu na sehemu ya miradi kujipatia-utajiri-wa-haraka. Tusiposhughulikia sababu za msingi za kukosekana kwa usawa inayoigawa mno jamii ya Malawi, tujiandae kwa matatizo zaidi.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.