Timu ya Soka ya Brazil Yazindua Kampeni Dhidi ya Ubaguzi wa Rangi

Katika video iliotolewa Jumatatu, Agosti 12, timu ya soka ya Grêmio of Porto Alegre ilileta pamoja baadhi ya wachezaji muhimu kwenye orodha ya majina yake, weupe na weusi, kwa majadiliano juu ya ubaguzi wa rangi. Mpango huo ulifanyika kusaidi mpango mpya wa FIFA, uliotekelezwa Mei mwaka huu na kupitishwa bila kupingwa, uliofanya adhabu dhidi ya ubaguzi wa rangi katika soka kuwa kali zaidi.

Wakati kampeni kwa ajili ya kuongeza uelewano na majadiliano dhidi ya ubaguzi wa rangi kwenye uwanja kumeongezeka katika miaka michache iliyopita katika Ulaya, swala mara chache hushughulikiwa ndani ya viwanja vya soka nchini Brazil.

Katika video, Ze Roberto, kiungo wa timu ya tricolor, aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Brazil, anaelezea jinsi yeye kamwe hajawahi kuwa mwathirika wa ubaguzi wa rangi kwenye uwanja, lakini kabla ya kuwa mchezaji wa mafanikio, alibaguliwa wakati wa mahojiano kwa sababu ya ngozi yake. Mjihami kiungo Matheus Biteco anakumbuka tukio kutoka utoto wake, wakati mlinda usalama katika maduka makubwa walikabiliana naye, baba yake, na ndugu yake Guilherme, pia mchezaji wa timu.

Kampeni ya timu ilifanya raundi kwenye mitandao ya kijamii kwa alama ashiria #azulpretoebranco (kumaanisha bluu, nyeusi na nyeupe, kufuatia rangi za timu).

[Viungo vyote vyaelekeza kwa kurasa ya lugha ya Kireno isipokuwa ibainishe vinginevyo]

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.