- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Tajikistan: Wapiga Kura Wana Haki ya Kujua Kama Wagombea “Wameshiba’ au ‘Wana Njaa’

Mada za Habari: Asia ya Kati, Tajikistan, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uchaguzi

Kama mtandao wa Sauti za Dunia ulivyoripoti [1], baadhi ya raia wa mtandaoni wanasema watampigia rais anayemaliza muda wake wakati wa uchaguzi wa Novemba 6 katika Tajikistan kwa sababu “kiongozi aliyeshiba ni bora kuliko aliye njaa”. Kutafakari juu ya hili, Salimi Aioubzod anadokeza [2] [tj] ni “huzuni” kuwa wapiga kura katika nchi wasiwasi wao zaidi ni kuhusu “shibe” au “njaa” ya mgombea urais= kuliko kuhusu jukwaa la mgombea. Hata hivyo mwanablogu anasema kuwa kama wapiga kura wanataka kujua namna mgombea wao “alivyoshiba” basi wana haki ya kujua hayo:

…itakuwa vizuri kama Tume ya Mpito ya Uchaguzi na kura ya maoni ya Tajikistan (CCERT) kuwataka wagombea wote wa urais kutangaza mapato yao ya kila mwaka na vyanzo vyake …

Kutangaza kwa umma mapato ya mgombea na asili yake, mali yao halisi, na akaunti ya benki yao itaruhusu [wapiga kura], ili kuona kama mgombea ni “kashiba” au “njaa” tupu…