Makala haya yalichelewa kuchapishwa kwa sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu. Yalipaswa kuchapwa mwezi Agosti 26, 2013.
Dhoruba kubwa ya kitropiki ya Maring ilisababisha mafuriko makubwa kuwahi kutokea katika Metro Manila na mikoa ya jirani nchini Ufilipino ambayo ilisababisha vifo vya watu 8, majeruhi 41, na 4 wakiwa hawajulikani walipo.
Kulingana na ripoti ya serikali, familia 125,348 zenye watu 602,442 ziliathirika na dhoruba hiyo. Kufikia Agosti 20 jioni, watu 40,837 bado walikuwa wamehifadhiwa katika vituo 198 vya uokoaji. Mafuriko yalifanya barabara kuu 65 kutopitika. Jumla ya maeneo 415 katika manispaa/miji 68 zilirekodi visa vya mafuriko. Idadi ya ndege 162 (59 ya kimataifa na 103 za ndani) kubatilishwa kutokana na dhoruba.
Wafilipino walitumia alama habari #maringPH na #floodPH kufuatilia hali ya mafuriko katika Manila na mikoa ya jirani. Zifuatazo ni baadhi ya picha kwenye mtandao wa Twita na Facebook ambazo zaonyesha kiwango cha maafa ya mafuriko.