- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Onesho la Mitindo Nchini Japan na Kauli Mbiu ya Kusitishwa kwa Matumizi ya Nguvu Dhidi ya Wanawake

Mada za Habari: Asia Mashariki, Japan, Sanaa na Utamaduni, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vijana, Wanawake na Jinsia
Image from last year's fashion show. The two models look like [1]

Picha ya maonesho ya mitindo iliyopigwa wakati wa onesho la mwaka jana. wapenzi hawa wanaonekana kwa nje wanafuraha, lakini mkono wa mwanamke huyu umefungwa pamoja na mkono wa mwanaume. Mkono wa kushoto wa mwanaume, ameshika bunduki isiyo halisi. Picha hii iliwekwa kwenye ukurasa wa Facebook wa Umoja wa Wanawake wa Asia (AWA).

The Umoja wa Wanawake wa Asia [2], shirika lisilo la kimaslahi la kutetea haki za wanawake, linategemewa kusimamia ; onesho la mitindo [3] [ja] siku ya tarehe 1 Desemba, 2013 likiwa na kauli mbiu isemayo “Mtindo wa Kukabiliana na Mfumo Kandamizi” yenye lengo la kuvuta hisia za watu katika kukabiliana na suala la matumizi ya nguvu dhidi ya wanawake. Onesho zima la mwaka jana linaweza kutazamwa hapa [4].