- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

“Nchi” Nzuri ya Afrika

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Kenya, Harakati za Mtandaoni, Maendeleo, Mahusiano ya Kimataifa, Sanaa na Utamaduni, Uandishi wa Habari za Kiraia

Katika toleo la wikii hii la Brainstorm [1], jarida la mtandaoni la Kikenya, Brenda Wambui hulaani masimulizi ya sasa kuhusu Afrika: “Afrika ni nchi”, “Afrika inapaa”, ‘”Mitindo ya Kiafrika.” Huchunguza jinsi Wakenya wanavyoweza kukomboa simulizi lao na kujiainisha kwa kuweka masharti yao wenyewe [2]:

Kama wenyeji wa Kenya ama nchi nyingine ile, tunafaa kujiainisha, kueleza msimamo wetu, kueleza tunayotarajia kutoka kwa nchi zingine tunazoshirikiana nazo, na kutaja yale tutakayokubali na yale ambayo hatutayakubali. Tunafaa kuunda utambulisho usiotegemea matarajio na dhana za wengine, kisha kuuegemeza. Kujitambulisha kwa maneno pekee yao hakutoshi, lazima ujitambulishe kwa vitendo vyako pia.