- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Kuwaokoa Akina Mama na Watoto Nchini Laos

Mada za Habari: Asia Mashariki, Laos, Afya, Uandishi wa Habari za Kiraia, Wanawake na Jinsia

Kundi la CleanBirth.org [1] lina nia ya kuboresha hali ya huduma ya afya ya uzazi katika baadhi ya vijiji vya Laos vijijini kwa kutoa vifaa vya kuzalisha, mafunzo ya wauguzi wapya na kuhamasisha kujitolea kwa wana kijiji. Katika taarifa ya hivi karibuni, kundi lilionyesha kwa nini wengi wa wana Lao vijijini huchaguakujifungua nyumbani badala ya kujifungua katika vituo vya afya. Miongoni mwa sababu ni ‘umbali na gharama za usafiri, matibabu duni, hamu ya kuwa karibu na familia, na hamu ya mazoea ya jadi ya kujifungua.