- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Huzuni na Hasira Mjini Kidal, Mali

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Mali, Ufaransa, Haki za Binadamu, Mahusiano ya Kimataifa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vita na Migogoro, Vyombo na Uandishi wa Habari

Mwanablogu Wirriyamu anaomboleza kuuawa kwa waandishi wa habari wawili wa ufaransa [1] [fr] mjini Kidal, Mali. Lakini kando na huzuni yake kubwa, Wirriyamu pia anajisikia hasira kwa kuona kaskazini mwa Mali inaendelea kutaabika tena kwa mashambulizi ya kigaidi. Anaandika [2] kuhusu hasira ya kimya chake kuhusu hali ya mambo:

Tant qu’il ne sera pas possible de patrouiller dans Kidal, tant que cette ville ne sera pas réellement dans une situation normale, ce genre d’assassinat continuera hélas à être possible. Si la paix doit avoir pour prix cette zone de non droit, alors (que les maliens me pardonnent) nous devons y renoncer au moins momentanément.

Iwapo jeshi haliruhusiwi kufanya doria huko Kidal, aina hii ya mauaji yataendelea kutokea. Kama kungelikuwa na amani halisi katika ukanda huu wa utaifa, gharama (marafiki zangu wa Mali mnisamehe) inaweza kuwa kujinyima amani kwa muda.