- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Filamu 14 za Mazingira zenye Kuvutia

Mada za Habari: Uingereza, Filamu, Mazingira, Sanaa na Utamaduni, Uandishi wa Habari za Kiraia

TVE (Televisheni inayohusika na Mazingira) yaonesha video 14 bora za washindani waliofika fainali kwenye shindano la kimataifa la filamu bora ya mazingira [1].

Washiriki kutoka sehemu mbalimbali za dunia wametengeneza filamu zinazochukua muda wa dakika 1 kwa kuzingatia mada zinazohusiana na mabadiliko ya hali ya hewa, maendeleo endelevu pamoja na bayoanuai.

Kila mmoja anaweza kupigia kura filamu aipendayo; mwisho ni tarehe 19 Desemba, 2013.