- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Ecuador: “Harakati ya Kiasili Itaendelea”

Mada za Habari: Amerika Kusini, Ecuado, Habari za wenyeji, Mazingira, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Utawala

“Serikali inaweza kuendelea na jitihada zake za kutufanya sisi kutosikika, lakini mapambano yetu hayawezi kushindwa. Bora kuna ukosefu wa haki, na kuwepo kwa tofauti kubwa kati ya mijini na vijijini kubaki, harakati ya kiasili itaendelea.”

Manuela Picq [1] alizungumza na Carlos Pérez Guartambel, kiongozi wa sasa wa Ecuarunari [2] [es] (Shirikisho la Kichwa la Ecuador), katika tukio lililo fadhiliwa na NACLA [3] (North American Congress on Latin America) na CLACS [4] (Center for Latin American and Caribbean Studies at New York University). NACLA [5]imechapisha nakala ya mazungumzo.