- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Nani ni Muislamu Halisi? -Hatari ya Madhehebu Madogo ya Waislamu Pakistan

Mada za Habari: Asia ya Kusini, Pakistan, Dini, Haki za Binadamu, Sanaa na Utamaduni, Uandishi wa Habari za Kiraia, Ubaguzi wa Rangi, Uhuru wa Kujieleza, Vita na Migogoro

Raza Habib Raja [1] wa Pak Tea House ana maoni haya:

‘Kosa’ kubwa nchini Pakistani ni kuwa kile ninachokiita, Muislamu asiye Muislamu. Kwa hiyo hata ukiwa Ahmedi, Shiite, na hata muumini wa Mtakatifu Sufi bado utaitwa Asiye Muislamu na baadhi ya watu.

Hilo linatuleta kwenye swali “nani ni Muislamu?” Raja anaeleza:

Kuuliza swali hili ni hatari na kujaribu kufafanua maana hasa ya Muislamu kunaweza kuwa hakuna maana yoyote na kunaweza kusababisha kutengwa kwa wengi wasiokuwa dhehebu la mtu anayeuliza swali hilo.