- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Masuala Matano ambayo Raia wa Brunei Wanahitaji Kuyajadili

Mada za Habari: Asia Mashariki, Brunei, Sanaa na Utamaduni, Uandishi wa Habari za Kiraia, Utawala

Teah Abdullah anaorodhesha [1] masuala matano ambayo raia wa Brunei citizens wanahitaji kuyajadili: Kuimarisha lugha halisi, ngono baina ya ndugu wa damu, maisha ya anasa, ulaji unaozidi kiwango wa “baga” [aina ya mandazi yenye nyama], utegemezi uliopitiliza kwa serikali. Anafafanua kwenye suala la mwisho:

…serikali ni sehemu muhimu katika maisha yetu ya kila siku, lakini kuitegemea sana ni tatizo kwa sababu inakuwa kama hatuwezi kutatua matatizo yetu binafsi. Tunajiongezea matatizo kwa kutegemea kuwa serikali itatatua matatizo madogo yanayotusibu kwenye maisha yetu.