- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Kuwasaidia Waathirika wa Tetemeko la Balochistan

Mada za Habari: Asia ya Kusini, Pakistan, Harakati za Mtandaoni, Majanga, Mwitikio wa Kihisani, Uandishi wa Habari za Kiraia, Wakimbizi

Zaidi ya watu 300,000 wameathirika kufuatia tetemeko la hivi karibuni [1] katika wilaya sita za Jimbo la Balochistan nchini Pakistan. Kashif Aziz [2] wa mtandao wa Chowrangi anatoa habari za namna ya kutoa msaada kwa waathirika wa tetemeko la Balochistan.