- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Korea Kusini: Mwandishi Msafiri, Utamaduni Tofauti, na Jamii ya Wageni

Mada za Habari: Asia Mashariki, Korea Kusini, Mawazo, Safari, Sanaa na Utamaduni, Uandishi wa Habari za Kiraia

John Bocskay, mwanablogu asiyeandika mara nyingi sana alifanya mahojiano [1] na mwandishi wa utalii Rolf Potts aliyetumia miaka kadhaa kwenye jiji la pili kwa ukubwa nchini Korea Kusini, Pusan, anasema:

Kila mtu niliyeonana naye katika vilabu vya wageni alidai kuwa mwandishi au msanii, lakini hungeweza kuona maandishi mengi au sanaa. Ilikuwa inaudhi na kuumiza, na sikuanza kuandika kuhusu Korea kwa namna ya maana mpaka nilipojifunza kuisogeza jamii hiyo ya wageni (marafiki na wafanyakazi wenzangu) karibu nami ili kuniwezesha kujifunza jiji hili, kwa mtazamo wa Kikorea.