- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Kampeni ya Mtandaoni ya Kudai Amani Nchini Msumbiji

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Msumbiji, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vita na Migogoro

Blogu ya Mozmaniacos [1] [pt] imezindua kampeni ya mtandaoni ya kudai amani nchini Msumbiji, kufuatia tishio la kuhatarisha amani iliyodumu kwa miaka 20 [2]. Kwa kutumia kiungo habari #MozQuerPaz [3] (#MozWantsPeace), watumiaji wa Facebook, Twitter, na Instagram waanza kuchangia picha zao pamoja na maoni yao kuhusiana na kampeni hii.