- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

India: Saa Nzuri Kapata Huduma za Afya Hospitalini kwa Punguzo la Bei

Mada za Habari: Asia ya Kusini, India, Afya, Sheria, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uchumi na Biashara

Kamayani [1] wa mtandao wa Kracktivist anasema kuwa dhana ya saa nzuri kupata punguzp la bei, ambayo ni maarufu sana kwenye vilabu vya pombe, mahotelini na hata kwenye majengo ya sinema, imeingia hadi kwenye sekta ya afya nchini India. Hospitali binafsi iliyoko Bangalore siku za hivi karibuni imekuwa ikitoa punguzo la bei kati ya asilimia 30-75 kwa huduma muhimu, ikiwa ni pamoja na uchunguzi, kufanyiwa vipimo vya x-ray na hata ushauri, wakati wa masaa yasiyo yasiyo na shughuli nyingi. Hosptali nyingine zinajiandaa kufuata mkondo huo hivi karibuni.