- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Uvumi Waenea Kwamba Putin Amefunga Ndoa Nyingine

Mada za Habari: Ulaya Mashariki na Kati, Urusi, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vichekesho, Vyombo na Uandishi wa Habari, RuNet Echo
Alina Kabaeva appears in a music video, 12 September 2010, screenshot from YouTube. [1]

Alina Kabaeva akionekana kwenye video ya muziki, Septemba 12, 2010, picha iliyopigwa kwenye video ya YouTube.

Kumekuwepo uvumi kwamba Vladimir Putin ana uhusiano wa kimapenzi na mcheza sarakasi wa zamani aliyezaliwa Uzbekistan Alina Kabaeva. Na kweli, uvumi huo ulikuwepo kabla ya talaka ya Putin, ambayo aliitangaza kwenye vyombo vya habari mwezi June 2013. Juma lililopita, tetesi ziliibuka kwa mara nyingine, na wakati huu “wapika majungu” wa RuNet wanabashiri kuwa Putin (umri miaka 60) na Kabaeva (umri miaka 30) hatimaye wanaweza kufunga pingu za maisha.

Habari zilianza na twiti [2] ya mchana wa Jumamosi:

Ninaambiwa kwamba Putin na Kabaeva wameoana leo katika nyumba ya watawa ya Iversky. Magari yote ya mji wa Valdai yako eneo hilo.

Ujumbe huu, ulioandikwa na mwanasheria Koloy Akhilgov, ulitwitiwa kwa zaidi ya mara 500, na kutzifanya blogu za ki-Rusi kupigana vikumbo kupata habari zaidi. Masaa mamchache baadae, Akhilgov aliripoti [3]:

Rafiki zangu, siwezi kuwa na habari za uhakika, lakini watu wa sehemu hiyo walisema kila kitu na kila mmoja amezuia kufanya chochote kuzunguka Iversky.

Akaunti ya twita inayomkejeli msemaji wa Putin, Dmitry Peskov, haikuchelewa kutwiti [4]:

Ndio, Vladimir Vladimirovich ameoa! Ingawa sio kwamba kamwoa Alina Kabaeva, lakini kauoa ufalme.

Ndani ya masaa machache tangu twiti ya kwanza ya Akhilgov, Dmitry Peskov alienda kwenye kituo cha televisheni cha TV Dozhd (TV Rain) na kukanusha uvumi huo [5], akiwalaumu wanablogu kwa kuandika haraka haraka bila ushahidi, na kuwashutumu watumiaji wa mitandao kwa “Kufanya mazoezi mtandaoni siku ya Jumamosi shauri ya kukosa cha kufanya.” Kanusho hili lililoonekana kuwa lisiloeleweka vyema lilikuza ziadi michapo ya mtandaoni. Kwa mfano, mtumiaji wa LiveJournalEgor Sedov alihoji [6] kwamba Peskov alikuwa amemwaga petroli kwenye moto wa tetesi hizo na kuzifanya ziwe habari kubwa zaidi.

Я этих слухов не слышал.  Зато теперь – услышал. Кому спасибо говорить? А г. Пескову, вот кому. Смолчал бы Песков – и слухи (даже если они и были) стихли бы сами собой. Теперь – нет. А вообще, Кабаева, вроде, мусульманка? Или нет? Если мусульманка, то возможно ли венчание?

Sikuwa nimezisikia kabisa tetesi hizo. Lakini sasa nimeshazisikia. Nimeshukuru nani? Bw. Peskov, ndiye wa kushukuru! Kama asingesema kitu, tetesi hizo (hata kama zingekuwa kweli) zingefifia zenyewe na kupotea. Lakini si sasahivi. Kitu kingine: Je, Kabaeva si ni Muislamu? Au sio? Kama ndivyo, hivi hapo harusi inawezekana kweli?

Akizungumzia upande huo buo wa dini kwa uwezekano wa ndoa kati ya Ptin na Kabaeva, mwanablogu mwingine alidodosa [7] kwamba Kabaeva alikuwa amebadili dini, ili aolewe na Putin.

Mwanablogu Pasha Businessman aliwasihi [8] wanablogu kuwa watulivu na kuacha kueneza uvumi usiothibitika:

Считаю все эти слухи выдумками. Кроме самих слухов подтверждений из других источников нет.

Ни одной фотографии, ни одного видео и так далее. Даже не важно как это комментирует пресс-служба. Кроме вбросов таблоидов и таблоидных журналистов никаких других фактов, что Путин встречается с Кабаевой нет.

Господа журналисты давайте не будем бегать впереди паровоза, получите факты, зафиксируйте, подтвердите из независимых источников а потом и публикуйте.

Ninafikiri uvumi wote huu ni wa kupikwa. Na ukweli ni kwamba, linapokuja suala la tetesi, hakuna kinachothibitishwa na vyanzo vingine. Hakuna picha hata moja, hakuna video hata moja, na kadhalika. Haina maana ofisi ya habari inasemaje. Ukiacha habari uchwara za magazeti, na waandishi wote wa magazeti, hakuna uthibitisho mwingine kwamba Putin [hata] amewahi kukutana na Kabaeva. Bwana, waandishi, hebu tusirukie gari kwa mbele. Kusanyeni taarifa, zifanyieni kazi, zithibitisheni kwa kutumia vyanzo huru, na kisha chapisheni.

Kwenye ukurafsa wake wa Facebook, mwandishi Natalia Gevorkyan alishangaa [9] kwa nini Ikulu ya Kremlin inapenda kufanya kila kitu kiwe “operesheni maalumu,” akibainisha namna Putin alivyosubiri uchokonozi wa magazeti ujue kila kitu kabla hajatangaza talaka yake.

Сколько лет не жил с женой, прежде чем сходить в театр на интервью о разводе? Теперь столько же лет проживет в браке, прежде чем о нем объявить? Может, правда, на Олимпийских играх…. Как-то логично-символично.

Ni miaka mingapi[Putin] hakuishi na mke wake kabla ya kwenda kwenye ukumbi wa mahojiano kuhusioana na talaka yake? Sasa ataishi miaka mingapi kenye ndoa hii kabla hajaitangaza rasmi? Labla, hata hivyo, wakati wa michezo ya Olimpik…kwa namna yoyote [inaweza kuwa] na mantiki ya mwonekano [kufunua jambo hili pale].

Habari ni kwamba uvumi kuhusu ndoa nyingine ya Putin ni uvumi tu. Lakini kama Gevorkyan yuko sahihi kwamba Putin anasubiri mazingira mengine yasiyotarajiwa, yenye halaiki ya watu wengi ndipo atoboe siri, basi tunaweza kusubiri mpaka kwenye Mashindano ya mwakani ya Olimpiki mjini Sochi.