- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Timu ya wanawake ya Mpira wa Kikapu ya Msumbiji Yafika Mbali

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Msumbiji, Michezo, Uandishi wa Habari za Kiraia, Wanawake na Jinsia

Kufuatia ushindi wa kishindo kwenye mashindano ya robo fainali (tazama habari zetu [1]), yaliyofanyika usiku wa jana timu ya mpira wa kikapu ya Msumbiji, wanawake, ilishinda nafasi ya kuingia kwenye Fainali za Mashindano ya Afrobasket usiku wa leo [2] dhidi ya washindi watetezi Angola. Kwa staili nyingine ya kurudi kwa ushindi dhidi ya Kameruni kwenye hatua ya nusu fainali [3], waliweza kujihakikishia nafasi kwenye Mashindano ya Dunia, na kuandika historia mpya ya michezo nchini humo.