- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Serikali ya Tanzania Yafunga Magazeti Mawili

Mada za Habari: Tanzania, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza, Utawala, Vyombo na Uandishi wa Habari

Serikali jana (terehe 27 Septemba, 2013) ilitangaza kuyafungia magazeti ya Mwananchi na Mtanzania [1] kutokana na kuandika habari na makala zilizoelezwa zina nia ya kusababisha wananchi wakose imani kwa vyombo vya dola na kuhatarisha amani.

Taarifa ya kufungiwa magazeti hayo ilisema;

Gazeti la MWANANCHI limefungiwa kutochapishwa kwa siku kumi na nne(14) kuanzia 27 Septemba, 2013…
Gazeti la MTANZANIA limefungiwa kutochapishwa kwa siku tisini (90) kuanzia tarehe 27 Septemba, 2013