- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Kwa nini Indonesia Haitakiwi Kupandisha Kima cha Chini cha Mshahara

Mada za Habari: Asia Mashariki, Indonesia, Habari za Wafanyakazi, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uchumi na Biashara

Rocky Intan aneleza kwa nini kupandishwa kwa kima cha chini cha mshahara [1] nchini Indonesia kutaathiri uchumi wa nchi hiyo:

Viongozi wa kitaifa na wale wa ngazi za chini lazima wapambane na shinikizo la baadhi ya viongozi wa vyama vya wafanyakzi wanaodai kupandishwa kwa kima cha chini cha mshahara. Ongezeko la kima cha chini limekuwa halihusiani na mfumuko wa bei, kinyume na madai ya waandamanaji. Zaidi, ongezeko hilo litasababisha matatizo zaidi ya wafanyakazi na hivyo kuathiri ushindani wetu katika uzalishaji unaotegemea nguvu kazi.