- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

India: Mgombea wa Uwaziri Mkuu na Historia yake ya Uhalifu

Mada za Habari: Asia ya Kusini, India, Sheria, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Utawala

“Je, mtu anaweza kuwa na historia ya uhalifu na bado akawa Waziri Mkuu wa India?” – anauliza Dr. Abdul Ruff [1] wakati anajadili uteuzi wa kiongozi wa mrengo wa kulia na Waziri Mkuu wa Gujarat Narendra Modi [2]. Ni mgombea wa Uwaziri Mkuu wa chama cha National Democratic Alliance katika uchaguzi mkuu ujao wa India wa mwaka 2014.