- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Daktari wa Peru ni Miongoni mwa Waathirika Waliopeza Maisha Westgate

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Amerika Kusini, Kenya, Peru, Habari za Hivi Punde, Uandishi wa Habari za Kiraia

Shirika la Habari la Andina limearifu [1] [es] siku ya Jumamosi, Septemba 21, 2013, kwamba daktari wa ki-Peru Juan Jesús Ortiz ni mmoja wa watu waliuawa katika shambulizi la kigaidi lililotokea katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, lilisababisha idadi ya vifo vya watu 59 [2] na wengine 175 wakijeruhiwa.

Hivi ndivyo Periodismo en Línea alivyotwiti habari hizo:

Daktari wa ki-Peru ni mmoja wa wahanga waliopoteza maisha katika shambulio la kigaidi lilitokea Kenya: Wizara ya Mambo ya Kigeni imethibitisha kwamba Juan Jesús Ortiz…