Kufuatia kuchomwa kwa makanisa, msichana mdogo katika Misri ya Juu alichora picha hii iliyonifanya nitiririkwe na machozi: pic.twitter.com/iymw3SF49R [1]
— daliaziada (@daliaziada) Agosti 15, 2013 [2]
Mtetezi wa haki za wanawake nchini Misri Dalia Aziada aliposti twiti hii baada ya makanisa kadhaa ya wakristo kuteketezwa katika maeneo mbalimbali nchini Misri [3] kufuatia operesheni ya kikatili iliyofanywa na jeshi Agosti 14 2013, iliyokusudia kuwatoa wafuasi wa chama cha Udugu wa Ki-islamu kutoka makao ya makambi katika mji mkuu wa Cairo [4], ambapo wamekuwa wakidai kurejeshwa madarakani kwa rais Morsi kwa wiki kadhaa.
Operesheni hiyo ya kuwaondoa wafuasi hao ilisababisha vifo vya watu wasiopungua 638 kwa mujibu wa serikali ya Misri. [5] Msemaji wa chama cha Udugu wa ki-Islamu amesema watu 2,000 waliuawa katika “mauaji hayo ya halaiki” [6].
Makumi kadhaa waliuawa mnamo Agosti 16 [7], wakati wafuasi wa Udugu wa ki-Islamu walipokuwa wakipambana na vikosi vya usalama katika “Siku ya hasira.”
Soma zaidi katika Habari zetu MaalumUmwagaji wa damu nchini Misri [8].