Kufuatia kuchomwa kwa makanisa, msichana mdogo katika Misri ya Juu alichora picha hii iliyonifanya nitiririkwe na machozi: pic.twitter.com/iymw3SF49R
— daliaziada (@daliaziada) Agosti 15, 2013
Mtetezi wa haki za wanawake nchini Misri Dalia Aziada aliposti twiti hii baada ya makanisa kadhaa ya wakristo kuteketezwa katika maeneo mbalimbali nchini Misri kufuatia operesheni ya kikatili iliyofanywa na jeshi Agosti 14 2013, iliyokusudia kuwatoa wafuasi wa chama cha Udugu wa Ki-islamu kutoka makao ya makambi katika mji mkuu wa Cairo, ambapo wamekuwa wakidai kurejeshwa madarakani kwa rais Morsi kwa wiki kadhaa.
Operesheni hiyo ya kuwaondoa wafuasi hao ilisababisha vifo vya watu wasiopungua 638 kwa mujibu wa serikali ya Misri. Msemaji wa chama cha Udugu wa ki-Islamu amesema watu 2,000 waliuawa katika “mauaji hayo ya halaiki”.
Makumi kadhaa waliuawa mnamo Agosti 16, wakati wafuasi wa Udugu wa ki-Islamu walipokuwa wakipambana na vikosi vya usalama katika “Siku ya hasira.”
Soma zaidi katika Habari zetu MaalumUmwagaji wa damu nchini Misri.
1 maoni