Mapigano Yalipuka Msikitini Baada ya Mhubiri Kumlaani el-Sisi

Mapigano yamelipuka kweeye msikiti wa Riyadh kati ya Wa-Saudi na wa-Misri baada ya mhubiri wa ki-Saudi kumlaani Waziri wa Ulinzi wa Misri Generali Abdel Fattah el-Sisi wakati mawaidha ya swala ya leo ya Ijumaa. Mapigano hayo, yaliyowekwa kwenye mtandao wa YouTube, yamesambazwa mno na kuzua mjadala mkali kwenye mtandao wa intaneti.

Video hiyo ya sekunde 46, ilipandishwa na watu mbalimbali kwenye mtandao wa YouTube, imekuwa ni mjadala wa siku miongoni mwa wanablogu wa ki-Saudi leo. Katika toleo moja liliwekwa mtandaoni na umum0707, limetazamwa zaidi ya mara 750,000 wakati wa kuandikwa kwa makala hii. Inaonyesha mwanaume aliyevalia mavazi ya ki-Saudi akivua kilemba chake, akimpiga mwanaume mwingine, Mmisri, ndani ya Msikiti wa Al Ferdous, baada ya Mmisri huyo kupinga kulaaniwa kwa el-Sisi. Ilikuwa kama ifuatavyo:

https://www.youtube.com/watch?v=un_l5tvTNe8

el-Sisi, ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu wa Kwanza wa Misri sasa, amehusika kwa kiasi kikubwa katika kumng'oa rais wa zamani Mohamed Morsi, mwanachama cha wa Udugu wa ki-Islamu.

Mohamed Al Omar aliweka kiungo hiki cha video katika mtandao wa twita na kusema [ar]:

@MdAlomar: هذا العراك هو الدليل الأول على الفوضى التي قد تحدث في حال نزل الخلاف من تويتر للشارع http://youtu.be/un_l5tvTNe8 #عراك_جامع_الفردوس

Mapigano haya ni ushahidi wa ghasia zitakazotokea kama yanayoendelea kwenye mtandao wa twita yatahamia mitaani.

Ibrahim Al Rasheed alisema mhubiri huyo hakuwa na haki ya kuzingumzia masuala ya Misri:

Watu wa Misri wanao ufahamu wa kutosha kuhusu mambo yao na haifai kwa mhubiri huyu kujiajiri kama mlezi wa wa-Misri.

Wengine wanatoa maoni ya namna ya kushughulikia watu kama mhubiri huyo katika siku za usoni.

Yazeed Al-Mogren anaandika:

Wakati mwingine, waumini wanapaswa kulivunja taya la muhubiri ili ajifunze na kuacha kuingiza maoni yake ya kisiasa kwenye mawaidha yake

Anaongeza:

Inasemekana mhubiri huyo amekamatwa. Je, wamefanyaje ng'ombe aliyenajisi msikiti na kuwapiga wa-Misri pale? Watakamatwa lini na kufunguliwa mashitaka?

Mwnaharakati Waleed Sulais haoni sababu ya hasira zisizo na sababu:

Tuseme hapana kwa matumizi ya nguvu. Tofauti za kisiasa zapaswa kuwa kwa amani, na kuchagua matumizi ya nguvu, kwa namna yoyote, haikubaliki

Anaongeza:

Kuwalaani wengine haikubaliki na kumpiga yeyote anayepinga hilo haifai. Watu wanastahili heshima.

Aziz anabainisha:

Na Mazeed Bandar anaunganisha nukta kupata maana kamili. Mhubiri anasemekana kuwalaani el-Sisi na Rais wa Syria Bashar Al Assad. Anatwiti:

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.