- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Makanisa Yashambuliwa Nchini Misri

Mada za Habari: Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Misri, Dini, Maandamano, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vita na Migogoro

David Degner aweka picha kutoka makanisa yaliyoshambuliwa na kuchomwa katika sehemu iitwayo Mallawi, Minya, Misri ya Juu hapa [1].

Anaandika:

Siku ya Ijumaa makanisa mawili katika kijiji cha Mallawi, jimbo la Minya, yalishambuliwa na kuchomwa moto.

Baada ya mashambulizi dhidi ya wafuasi wa Morsy  ambapo zaidi ya watu 600 walifariki, wafuasi wa Morsy walikusanyika baada ya swala ya Ijumaa wakavamia na kuchoma makanisa mawili, na baadhi ya maduka yanayomilikiwa na wakristo katika kijiji cha Mallawi.

Watu walikuwa katika makundi pia walishambulia na kuiba vitu kwenye chumba cha makumbusho kijijini humo, na benki, maduka na makanisa mengine 10 jimboni humo.

Anaweka video hii, inayoonyesha Kanisa la Kiinjili, kijijini humo likiwaka moto: