- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Iran: Waziri Mpya wa Kigeni Yupo Kwenye Mtandao wa Facebook

Mada za Habari: Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Iran, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Utawala

Waziri mpya wa Uhusiano wa Kimataifa wa Iran Mohammad Javad Zarif ana ukurasa wa Facebook [1] ambapo huutumia kujibu maswali. Anasema [2] “Mimi na watoto wangu huuhuisha (kuweka habari mpya) ukurasa huu.” Ukurasa huo una zaidi ya wafuatialiaji 79,854 walioupenda (wakati wa kutafsiriwa kwa posti hii). Mtandao wa Facebook hudhibitiwa nchini  Iran lakini ndio uliotumiwa [3] na wagombea wote wa urais katika uchaguzi uliopita.