- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

China: Kisasi au Haki?

Mada za Habari: Asia Mashariki, China, Sheria, Uandishi wa Habari za Kiraia, Utawala

Kashfa ya ngono [1] ya hivi majuzi inayowahusisha majaji wawili maarufu wa Shanghai iliwekwa hadharani na mfanyabiashara Ni Peiguo anayeamini kuwa mmoja wa majaji hakutoa hukumu ya haki katika kesi ya kampuni anayohusika nayo. Alichukua uamuzi wa kulipiza kisasi kufuatia hasara ya fedha kwa kumfuatilia hakimu kwa mwaka na hatimaye kufichua kashfa yake ya ngono. Mtandao wa China Beat ulisaili [2] maoni ya raia wa mtandaoni juu ya kisasi cha Bw. Ni, ambayo ina ufanisi zaidi kuliko kujaribu kukata rufaa dhidi ya kesi.