- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Tamko la Kurekebisha Sheria Zinazokwaza Uhuru wa Vyombo vya Habari Nchini Vietnam

Mada za Habari: Asia Mashariki, Vietnam, Haki za Binadamu, Maandamano, Sheria, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza, Vyombo na Uandishi wa Habari

Zaidi ya wanablogu 60 wa Ki-vietinam walitia saini tamko la pamoja [1] kuitaka serikali ya Vietnam kuboresha rekodi ya haki za binadamu na ahadi wanapowania uanachama katika Baraza la Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu:

Serikali ya Vietnam pia inahitaji kutathmini  hali ya haki za binadamu katika nchi hiyo na wa-Vietinamu pia wana haki ya uhuru wa maoni na kujieleza, ikiwa ni pamoja na masuala haya.

Kama watetezi wa uhuru wa kujieleza nchini Vietnam na wahanga wa ukiukwaji wa haki za binadamu kwa sababu ya harakati zetu, sisi twaona mgombea Vietnam kwa Baraza la Haki za Binadamu kama jukwaa kwa ajili ya majadiliano ya kujenga haki za binadamu katika nchi yetu.