- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Shindano la Wanablogu wa Kiafrika wenye Fikra Pevu.

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Botswana, Maendeleo, Teknolojia, Uandishi wa Habari za Kiraia

Mtandao wa Africa Brains watangaza [1] Shindano la Wanablogu wa Kiafrika Wenye Fikra Pevu watakaowania kitita cha dola Hamsini ($50).

Ni muda muafaka wa kutangaza mada ya kwanza, ambayo ni “Teknolojia imekuwa na ushawishi gani katika elimu yako?”
Tufahamishe hali ya upatikanaji wa teknolojia ulipokuwa shuleni au chuoni? Tangu uanze kutumia teknolojia, kumekuwa na mabadiliko? Wewe na wanafunzi wenzako mmekuwa na ufahamu wa zaidi wa teknolojia kuliko walimu wenu?