- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Peru: Mchezaji wa Kandanda Afariki Dunia Uwanjani

Mada za Habari: Amerika Kusini, Peru, Michezo, Uandishi wa Habari za Kiraia

Dakika tano kabla ya kumalizika kwa mchezo kati ya timu zaReal Garcilaso [1] na Sporting Cristal [2], mchezaji nyota wa timu ya Sporting Cristal mwenye miaka 18 Yair José Clavijo alipata mshituko wa moyo na akapoteza maisha. Madaktari wa timu hiyo walijaribu bila mafanikio kunusuru hali yake akiwa kwenye sehemu ya kuchezea katika uwanja wa Manispaa ya Urcos [3], katika mkoa Cusco [4].

Mtangazaji wa zamani wa kandanda Elejalder Godos [5][es] aliungana na watumiaji wa mtandao wa Twita ambao waliamua [6] [es] kuingia kwenye mtandao huo kuonyesha hisia zao kuhusu habari hizo za kusikitisha:

Rambirambi zangu kwa familia ya Yair Clavijo kwa kifo cha ghafla cha mchezaji kinda wa timu ya Sporting Crital akiwa uwanjani.