- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Maandamano ya Kudai Uchaguzi nchini Madagaska Yasababisha Vurugu

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Madagaska, Mahusiano ya Kimataifa, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uchaguzi, Utawala
Protests in Antananarivo, Madagascar on July 22, 2013 photo via MaTV [1]

Maandamano jijini Antananarivo, Madagaska tarehe 22 Julai, 2013. Picha kupitia MaTV

Blogu ya Vola R ya Ma-Laza inaandika kwamba watu 7 walijeruhiwa [1] [fr] kufuatia matumizi ya nguvu yaliyofanywa na polisi dhidi ya waandamanaji waliokuwa wanadai kufanyika kwa uchaguzi mjini Antananarivo, Madagaska. Chama kinachoongoza maandamano kinasema kwamba utawala uliopo hauna dhamira ya kuitisha uchaguzi mwaka huu na kwamba serikali imeng'ang'ania madarakani. Kiongozi wa chama hiko alidaiwa kukamatwa kufuatia maandamano hayo.