Benin: Kampeni ya Kusaka Wahalifu Yawagawa Wananchi

[Viungo vyote vinaelekeza katika lugha ya Kifaransa]

Kampeni ya Djakpata, iliyozinduliwa mapema mwezi April 2013 na Wizara ya mambo ya ndani, Ulinzi na Dini ya Benin, inadhamiria kuwasaka wahalifu wote wanaojihusisha na shughuli zote zisizo halali na ambazo zinaweza kuleta usumbufu kwa watu wa Benin. Hata vivyo, katika siku chache zilizopita, maoni ya watu yamekuwa tofauti mno kuhusiana na kampeni hii.

Safety in Benin by Felix Krohn on Flickr CC-BY-NC

Usalama nchini Benin. Picha na Felix Krohn kutoka mtandaO wa Flickr CC-BY-NC

Katika blogu yake, Illassa Benoit alimkariri Charles Toko, ambaye ni mfanyabiashara kutoka Benini:

Opération Djakpata. [Djakpata serait] un serpent qui avale des gens. Un Boa ? Hum…très peu au Sud Bénin, sinon inexistant. Un Anaconda ? Ça n’existe pas en Afrique. Une vipère ? Ça n’avale pas un homme. Or, à en croire certaines langues au sud du Bénin, Djakpata est un serpent qui avale des hommes. Ce qui est faux. Donc l’opération en elle-même est fausse au départ. Les développements le confirment.
Au départ, une manipulation. On a sorti des engins qui ne sont pas destinés au Bénin. Au fait, ce sont des engins que le Bénin loue à l’ONU. Mais depuis 2006, le mensonge est considéré par le gouvernement comme une communication par excellence. Alors, on s’y adonne. On nous montre des mini chars, des 4X4 de patrouille, des canons, …. Comme d’habitude, c’est pour mentir.

Kampeni ya Djakpata inaweza kuwa ni nyoka amezaye watu. Au ni yule nyoka Boa? Hmm… (nyoka huyu) ni nadra sana Kusini mwa Benini, na bila shaka hayupo kabisa. Anaconda? Hayupo barani Afrika. Ni Kipiribao (Viper-aina ya nyoka mwenye sumu kali)? Nyoka huyu hawezi kummeza mwanadamu. Haijalishi, kama unawaamini watu fulani kutoka Benini ya Kusini, kampeni ya Djakpata ni nyoka mmeza watu. Hii siyo kweli. Kwa hiyo, kampeni yenyewe toka mapema imeonekana kuwa na mapungufu. Maendeleo yake yatalithibitisha hili.
Tokea awali kumekuwa na ubabaishaji. Vitendea kazi ambavyo vimekuwa vikitumika havikukusudiwa kwa Benini. Na kwa kweli, hivi ni vitendea kazi ambavyo viliazimwa kutoka Uingereza. Hata hivyo, tangu mwka 2006, serikali imekuwa ikiamini kuwa kudanganya ni namna nzuri sana ya mawasiliano. Kwa hiyo wanaitumia sana. Wanatuonesha vifaru vya wastani, magari ya kuweka doria ya 4×4, mizinga…. Kama kawaida, haya yanafanyika kama namna ya kuhadaa tu.

Mtukio kwa Ufupi

Serikali ya Rais Boni Yayi siku za hivi karibuni ilianzisha kampeni iliyopewa jina la ‘djakpata’. Kwenyetovuti ya Adjinakou, Gathum Gbaguidi alifafanua kwa ufupi muktadha wa kampeni hii ya Ulinzi:

” Djakpata 2013 ” c'est le nom de l'opération lancée lundi dernier par le ministre de l'intérieur, de la sécurité publique et des cultes, Benoît Dègla, sur l'esplanade du stade de l'Amitié de Cotonou. Djakpata, qui est le nom donné à la vipère en langue fon, a été attribué à l'opération qui vise à aller à l'assaut des malfrats de tout acabit dont les jours sont désormais comptés, à moins qu'ils changent de métier. Cette opération conjointe de toutes les forces de sécurité et de défense a mobilisé des milliers d'agents des forces de sécurité et de défense, des véhicules légers de patrouille, des véhicules spécifiques de maintien d'ordre et des blindés légers. Ainsi donc, pendant trois mois, cette grosse artillerie va mener une lutte sans merci contre l'insécurité sous toutes ses formes dans toutes les localités du pays en commençant par Cotonou et ses environs.

“Djakpata 2013” ni jina la kampeni iliyozinduliwa rasmi Jumatatu iliyopita na Benoit Degla ambaye ni Waziri wa mambo ya Ndani ya Ulinzi wa Umma na dini katika uwanja wa,katika jukwaa la Uwanja wa Urafiki wa Cotonou. Djakpata, ambalo ni jina la Kipiribao katika lugha ya Fon ( watu wa Kusini mwa Benini), ndilo jina iliyopewa kampeni ambayo ina lengo la kuwafuatilia wahalifu wote ambao siku zao tayari zinahesabika, ili angalau kwa kiasi fulani wabadili namna zao za maisha. Kampeni hii inayosimamiwa na vyombo vya ulinzi na usalama kwa pamoja wameshawaleta pamoja maelfu ya maofisa wa usalama na ulinzi, magari ya doria, magari kwa ajili ya kutolea taarifa pamoja na magari ya kijeshi. Kwa hiyo, kwa miezi mitatu, vyombo hivi vya usalama vitaongoza mapigano yasiyo ya huruma na kukosekana kwa usalama katika maeneo mbalimbali ya nchi kuanzia Cotonou na maeneo ya karibu.

Katika blogu yake, François Django alifafanua malengo ya kampeni hii:

Sur une patrouille mixte des forces de l'ordres,toute l'armée béninoise se donne la main pour lutter contre l'incivisme et l'insécurité au Bénin. Désormais la nuit appartient à l'armée béninoise. Ne circule plus qui veut mais qui possède des preuves évidentes pour se défendre.

Un processus salué par la population béninoise, car vivre dans la sécurité viens la décharger des gouffres de la misère.

Le souhait est que cette opération dure dans le temps et s'élargisse à toute les autres villes. Et que la paix soit toujours l'ami du Bénin, exemple de démocratie dans la sous région et dans le monde entier.

Jeshi lote la Benini linasaidia kukabiliana na vitendo viovu dhidi ya wanajamii na hali ya kukosekana kwa usalama nchini Benini kwa kutumia doria inayojumuisha vyombo mbali mbali vya kisheria na kiulinzi. Kuanzia sasa, usiku unabaki kuwa ni wa jeshi la Benini. Hakuna atakayeruhusiwa kutembea nje wakati wa usiku kiholela, isipokuwa kwa wale tu watakaokuwa na kibali sahihi cha kujilinda wao wenyewe. Mchakato huu ulipokewa na watu wa Benini, kwani kuishi kwa amani kunapunguza ukali wa hali ya umasikini iliyopo.

Matumaini yaliyopo ni kuwa, kampeni hii itakuwa endelevu na kusambaa katika miji mingine yote. Na hivyo daima amani itakuwa ni rafiki wa watu wa Benini, ni mfano wa demokrasia nchini Benini na ulimwenguni kote

Video hii inaonesha uzinduzi wa kampeni hii.

Benin: Benoit Degla akiizindua kampeni ya Djakpata na actubenin

Katika mitandao ya kijamii, watu wa Benini hawaoneshi kuiunga mkono kampeni hii.

Katika Twita, mtumiaji wa intaneti alitania:

@shimkmb: J'ai reve que les policiers de Djakpata m'embarquaient

@shimkmb: Niliota kuwa polisi wa Djakpata waliniswaga niwafuate

“@Arlus_BDS: @jessebonheur: ne m'envoi plus jamais d'invitation de path , tu veux Djakpata chez toi ou quoi ?”

“@Arlus_BDS: @jessebonheur: Usinitumie tena mialiko ya Path, unawataka Djakpata nyumbani kwako au?”

“@Jules_Roland: “Opération Djakpata” tourne au fiasco ! C'est triste mais c'est à mourir de rire… #Bénin http://t.co/ep72vPhXlV

“@Jules_Roland : “Kampeni ya Djakpata” inaenda kushindwa! Inasikitisha lakini inakufanya ufe kwa kicheko…#Benin http://t.co/ep72vPhXlV

@jcommejasmine: Plus rien ne va ds ce pays… Ca nous parle d'”Opération Djakpata”, mais ca se fait braquer aussi! On est ou la?

@jcommejasmine: Hakuna kinachowezekana katika nchi hii… wanaongelea “Kampeni ya Djakpata”, lakini hata hii haifiki mahali! Lengo lake ni nini haswa?

@LaTeam_229: Les USA ont Les Experts Manhattan, Les Experts Miami nous #AuBénin on a #DJAKPATA

@LaTeam_229: Marekani wana wataalamu wa Manhattan, wataalam wa Miami #AuBénin {huku Benini] tuna #DJAKPATA

@EAHOUNOU: Ou on est t-on avec l'Opération #DJAKPATA :Braquage hier vers #Missèbo à #Cotonou en plein jour… Qd la Police pense politique … #le229

“@EAHOUNOU:Imetufikisha wapi kampeni ya DJAKPATA inayoendelea Missèbo, Cotonou mchana kweupe… pale polisi wanapowaza kwanza siasa … #le229

“@CDjidjoho: #AuBenin quand djakpata te vois la nuit il te frappe d'abord !!! Avant de te demander des explication

“@CDjidjoho: #AuBenin [huku Benini] polisi wa djakpata wakikukamata usiku, wanakupiga kwanza kabla ya kukupa fursa ya kujieleza

Pamoja na kampeni muhimu za kuwajulisha watu kuhusiana na kampeni ya Djakpata, hadi sasa, ufaninisi wa kiujumla wa mpango huu umeonekana kuleta matokeo yanayokinzana mpaka hapo ilipofikia.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.