2 Julai 2013

Habari kutoka 2 Julai 2013

Misri: Wasalafi Washambulia Makazi ya Washia, Wanne Wauawa

Watu wanne nchini Misri ambao ni wafuasi wa imani ya Shia wameuawa leo nchini Misri mara baada ya nyumba waliyokuwa wanakutania kushambuliwa na Waislam wenye msimamo mkali, shambulio hili linafuatia wiki mbili za uchochezi dhidi ya waumini wa Shia. Kwa mujibu wa taarifa za awali, nyumba ambayo waumini hao wa Shia waliyoitumia kukutania, iliyopo huko Giza, Cairo, ilishambuliwa na kuchomwa moto. Kwa mujibu wa taarifa za habari za Al Badil, shuhuda mmoja alikaririwa akisema kuwa mmoja wa watu waliouawa alichinjwa na wengine watatu walijeruhiwa vibaya vichwani mwao. Tukio hili la kutisha lilizua ghadhabu kubwa mtandaoni.